February 6, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Spika aitaka Serikali iweke maeneo ya kihistoria ya Papa Leo XIV

Papa Leo XIV

 

SPIKA wa Bunge Mussa Zungu amesema kuna haja serikali ikaweka maeneo ya kihistoria Tanzania, ambayo Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV aliishi alipokuwa nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Spika Zungu ametoa kauli hiyo leo 6 Februari 2026, muda mfupi baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof Kitila Mkumbo kumaliza kufanya majumuisho ya hoja mbalimbali za wabunge kwenye hotuba yake kuhusu Mpango Elekezi wa Muda mrefu wa miaka 25 (2026/27 hadi 2050/51), Mpango wa Nne wa Maendeleo wa miaka mitano (2026/27 hadi 2030/31) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2026/27.

Zungu amesema Papa Leo ameishi Tanzania na amekuja mara kadhaa maeneo ya Morogoro, Dar es Salaam na Songea mkoani Ruvuma, lakini wengi hawajui kuhusu historia hiyo.

Aidha wapo marafiki wa Papa Leo, zipo nyumba alizoishi na hata mabenchi aliyokuwa anakalia kanisani, ni vyema vikawa sehemu ya kutengeneza maeneo ya historia ili kuvutia watalii wa kidini wanaokuja nchini.

Papa Leo XIV alikuja Tanzania mwaka 2003, kutembelea jumuiya za Waagustino Tanzania yeye akiwa mkuu wa shirika ulimwenguni. Na kati ya shughuli alizozifanya, alikuja akafikia Mahanje kule Songea mkoani Ruvuma

About The Author

error: Content is protected !!