December 11, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Buriani Jenesta Mhagama

 

JENESTA Mhagama, mbunge wa Peramiho, mkoani Ruvuma (CCM), amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Bunge imeeleza kuwa Jenesta amekutwa na umauti leo, tarehe 11 Desemba 2025, mjini Dodoma.

Hata hivyo, taarifa ya Bunge iliyotolewa na Spika wake, Mussa Azzan Zungu, haikueleza Jenesta alikuwa anasumbuliwa na maradhi gani. 

Mbunge huyo wa siku nyingi katika Bunge la Muungano, amewahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya Bunge kwenyewe na serikali.

Mathalani, Jenesta amewahi kuwa Mwenyekiti wa Bunge; Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge na Vijana; Waziri wa Utawala Bora na Waziri wa Afya.

About The Author

error: Content is protected !!