December 2, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Samia: Oktoba 29 walitaka kupindua dola ninayoiongoza

Rais Samia Suluhu Hassan

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema matukio ya vurugu yaliyotokea kuanzia 29 Oktoba 2025 siku ambayo uchaguzi mkuu ulifanyika na siku zilizofuata yalikuwa matukio ya kutengenezwa yaliyolenga kuangusha dola ya nchi yetu. Anaripoti Mwandish Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ameyasema hayo leo 2 Disemba 2025 akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam na kusema lile jambo lilikuwa la kupangwa na vurugu zile zilidhamiria makubwa ni mradi mpana sana wa wenye nia ovu

“Lililotokea ni tukio la kutengeneza na waliolipanga walidhamiria kuangusha dola ya nchi yetu”

Rais Samia ameeleza kuwa vijana walioshiriki waligeuzwa makasuku na kuimbishwa kabisa maneno kama ‘yaliyotokea Madagascar na huku yatokee’ huku akieleza kuwa vijana hao ukiwahoji yaliyotokea Madagascar ni yapi hawajui.

“Vijana wetu waligeuzwa makasuku na kuimbishwa kabisa, yaliyotokea Madagasca na huku yatokee kabisa lakini ukimvuta kijana yule ebu niambie Madagasca kulitokea nini? Hajui unataka hapa kitokee nini? hajui kwahiyo lile lilikuwa jambo la kupangwa”

Pia amesema vijana waliimbishwa wimbo wasioujua wanasema wanadai haki je ni haki gani wanayoitaka je hiyo haki hawakuweza kuidai kwa njia nyingine mpaka waingie njiani wakafanye vurugu “walipwe wakachome vituo” na kusema wengine wanadai waliingia njiani kutokana na ugumu wa maisha.

About The Author

error: Content is protected !!