WAKATI vyombo habari nchini Tanzania vikitajwa kurudi nyuma kwa kushindwa kuripoti au kuandika matukio yenye maslahi kwa umma msemaji wa serikali amevisifia kwa weledi. Anaandika Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Ripoti ya YearBook ya 2020 kuhusu ubora wa maudhui ya vyombo vya habari nchini ya mwaka 2020 ileeleza hali ya vyombo vya habari nchini kuwa imedumaa.
“Huenda udumavu huu pia ukawa umechangiwa na uwezo mdogo wa waandishi wa habari na wahariri, kukamatwa kwa vyombo vya habari na wadau wenye maslahi yao kutoka serikalini, wanasiasa, na
wafanya biashara na pengine hofu inayoendelea miongoni mwa wanahabari na hata vyanzo vya habari kuhusu kutoa maoni kosoaji kwa serikali”
Sifa hizo zilizomwaga na msemaji wa serikali zimekuja baada ya vyombo vya habari nchini kushindwa kuripoti kwa undani matukio ya tarehe 29 Oktoba 2025 siku ambayo Tanzania ilifanya uchaguzi. Siku hiyo hiyo kuliibuka maandamano ya Gen Z.
Maandamano hayo yalipelekea vyombo vya ulinzi na usalama kunyanyua mitutu na kusababisha mauaji ya wananchi.
Waandishi wa habari nchini wameshindwa kuhoji kwanini mpaka leo kuna familia zinatafuta miili ya ndugu zao kwa wale wenye uhakika kuwa ndugu zao wamefariki kama ilivyofamilia ya Maneno Selanyika aliyekuwa Mwandishi wa New Habari.
Aidha wale wasiokuwa na uhakika ndugu zao wapo au hawapo wanahangaika kwenye vituo vya polisi kuulizia ulizia kama ndugu zao wapo selo au la.
Waandishi wa habari sio kama hawaoni kuwa hiyo ni habari wanahofia msumeno mkali wa sheria zilizowekwa ili kuwadhibiti.
Chombo cha habari kinaweza kufungiwa endapo tu kimeendeka habari ya upande mmoja mathalan chombo cha habari kiwe kima taarifa ya idadi ya watu waliokufa kwenye maandamano habari hiyo ikichapishwa au kiripotiwa bila kuthibitishwa na mamlaka husika.
Vyombo vya habari Tanzania haviwezi kufanya uchunguzi kwa sababu ya sheria kama hizi na nyingine lakini haibadilishi ukweli wa kwamba vimeshindwa kutekeleza wajibu wake wa msingi.
Kishindwa huku matokeo yake sasa wananchi hawana imani na vyombo vya ndani badala yake wanaamini BBC, Aljazeera, CNN na mitandao ya kijamii.
Serikali ikiona kama ukimya au kutowajibika kwa vyombo vya habari ni manufaa upande wake basi ombwe na vyombo hivyo litazibwa na uandishi wa habari wa kiraia ambavyo vishaanza kazi.
Na itapelekea vyombo vya habari kufa kwa kukosa wasomaji, watazamaji au wasikilizaji vitashindwa kujiendesha hata venye ruzuku havitakuwa na tija.
Sasa ni wakati wa serikali kupima uwezo wa vyombo vya habari kwa weledi wa kuripoti matukio yote sio tu yale yanayopendezwa nayo haya yale wasiyoyapenda.
ZINAZOFANANA
Maswali tata ya Wahariri kwa Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba
Rais wa zamani wa Brazil, anaanza maisha mapaya gerezani
Heri ya siku ya kuzaliwa kwa Polepole, ni siku 51 tangu ametekwa