November 25, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Siachi kusoma gazeti la MwanaHALISI – Profesa Kabudi

 

WAZIRI Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi, amesema kuwa miongoni mwa magazeti ambayo hawezi kuacha kusoma ni pamoja na MwanaHALISI linalozalishwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Prof. Kabudi ameyasema hayo leo tarehe 25 Novemba 2025, wakati wa mkutano wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mwigulu Nchemba alipokutana na wahariri wa vyombo vya Habari mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yake Prof. Kabudi alisema kuwa kupitia maandiko mbalimbali anapokosolewa analibeba kwa umakini na kujisahihisha kwa kuwa ni moja ya majukumu ya chombo cha Habari.

“Miongoni mwa magazeti ambayo siachi kusoma ni MwanaHALISI, mnaponipongeza nashukuru wanaponikosoa nalibeba kwa umakini inamaana ni kioo najisahihisha”- alisema Prof. Kabudi.

Ikumbukwe gazeti la MwanaHALISI utoka kila siku ya Alhamisi

About The Author

error: Content is protected !!