Thabo Mbeki
TAASISI ya Thabo Mbeki imetoa risala za rambirambi kwa familia zilipoteza wapendwa wao, kutokana na vurugu za uchaguzi mkuu wa 29 Oktoba 2025, nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
“Wakfu unatoa taarifa hii kufuatia kutafakari kina na ya uchungu kwa uchaguzi mkuu uliofanyika Tanzania tarehe 29 Oktoba2025.
“Mlezi, Bodi ya Wadhamini na Wakfu wote wa Thabo Mbeki, tunatoa pole nyingi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao wakati huu, vurugu zilizotokea dhidi ya wananchi kufuatia uchaguzi huo. Tunaomba pia kwa ajili ya uponaji wa haraka kwa majeruhi wote wa kipindi hiki cha misukosuko,” inaeleza taarifa hiyo.
Taassisi ya Thabo Mbeki inasema, timu za waangalizi wa uchaguzi huo (The Election Observer Missions-EOMs) za kikanda na mashirika, SADC na AU, yametoa taarifa inayotukatisha tamaa kuhusu mwenendo wa uchaguzi uliovyofanyika.
Kwa pamoja, timu za waangalizi zilihitimisha kuwa uchaguzi mkuu wa Tanzania uligubikwa na kasoro kadhaa na ukiukwaji wa misingi ya viwango vya chaguzi za kidemokrasia.
Taarifa inasema, wapigakura nchini Tanzania hawakuwa huru kutimiza takwa lao la kidemokrasia.
“Kwa hiyo, waangalizi wa SADC na AU wanasema wazi kuwa uchaguzi wa Rais na matokeo ya ubunge yaliyotangazwa sio taswira ya kweli ya mapenzi ya watu Watanzania,” anaeleza.
Anaongeza, Wakfu kwa kuzingatia taarifa za ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi huo, tunahitimisha kwamba uchaguzi wa Tanzania ulikuwa na mapungufu kwenye kanuni na miongozo inayosimamia uchaguzi wa kidemokrasia katika viwango vya kimataifa.
Ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi ulisema “wapiga kura wa Tanzania hawakuweza kutumia uhuru na dhamira yao ya kidemokrasia,” taasisi ya Mbeki ilisema na kuongeza, “Nchi hiyo inahitaji mwanzo mpya tena haraka.”
“Hii imesababisha hitimisho kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa sasa haina serikali halali, ikionyesha badala yake kwamba utawala wa sasa umelazimishwa kwa watu kupitia mchanganyiko wa nguvu na njia za ulaghai,” Wakfu huo umeeleza.
Taasisi hiyo imesema kuwa msingi wao unashikilia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watu wake kwa heshima kubwa, na kuwaheshimu kama marafiki wa kweli na washirika.
Taarifa hiyo imerejelea wito wa maridhiano uliotolewa, lakini haraka ikasema, “Matokeo chanya yanaweza tu kupatikana kupitia ukweli, ujumuishaji wa kila mmoja na uhuru wa mazungumzo ya kitaifa.”
Taarifa ya taasisi hiyo, iliyosainiwa na mtendaji wake mkuu, Max Boqwana, imeitaka Serikali ya Tanzania, kujibu maswali muhimu kama vile nini kilikoseka na kipi kinastahili kufanywa, kurejesha hali kuwa ya kawaida na kufikia haki, maridhiano na umoja wa kitaifa.

Hali hii inazidishwa na taarifa zinazoendelea za kutatanisha za unyanyasaji wa kimfumo dhidi ya wapinzani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ikiwa ni pamoja na utekaji na mauaji.
Kama ilivyo kwa waafrika wengi, “Wakfu wetu unachukulia kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na watu wake kwa heshima kubwa, na kuwaheshimu kama marafiki wa kweli na washirika.
“Katika sherehe zetu za Siku ya Afrika zilizofanyika mapema mwaka huu Morogoro na Dar es Salaam, tulihisi kwamba taifa halijatulia.
“Tunaona kuwa ni fursa nzuri kukumbusha yale ya marehemu, Rais Julius Kambarage Nyerere, asiyeweza kushindwa kama mmoja wa viongozi wetu. Tunabaki kuwa walinzi wa urithi wake na pia sana chochote kinachochafua.”
Wakfu unasema, “Watu wa Tanzania wana deni la matokeo haya kwa Marehemu Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere, na kwa Waafrika wenzao kote barani Afrika.”
ZINAZOFANANA
Ripoti yetu kuhusu Tanzania imezingatia weledi – CCN
Mzimu wa Oktoba 29 unavyoitesa Serikali
Rais Samia atetea Tume yake