RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema uteuzi wa Mwigulu Nchemba umepitia ushindani mkubwa na baada ya kuona vigezo alivyonavyo katika kuitumikia nchi hii na katika kuwatumikia wananchi wa jamhuri wa muungano wa Tanzania akaibuka kuwa mshindi zaidi ya wengine. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Ameyasema hayo leo tarehe 14 Novemba 2025 kwenye hafla fupi ya kumuapisha waziri mkuu wa Tanzania Mwigulu na ametoa pongezi kwake kwa kuibuka mshindi kutokana na sifa alizonazo zilizo washinda wengine
Pia amesema kazi zake na maelekezo yote yapo kwenye katiba lakini amemkabidhi vitabu vinavyoeleza majukumu yake na mambo yote anayotakiwa kuyaangalia na kusema kuwa amepokea kijiti kutoka kwa Waziri mkuu mstaafu Majaliwa ambaye amefanya kazi nzuri kwa yale Tanzania wanayojinadi leo.
Samia ameongeza kuwa yapo mengi waliyo ahidi wananchi hivyo ni wajibu wake kuhakikisha kasi ya yale waliyoyaahidi yanatekelezwa ndani ya mda mfupi na kusema vishawishi ni vingi ila ana imani naye.
ZINAZOFANANA
Mwigulu kuapishwa kesho Ijumaa
Tuache kiburi, tuliokoe taifa – Mwabukusi
Ngoma bado mbichi, Lissu aibuka na pingamizi jipya