October 22, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Lissu aweka pingamizi lingine, mahakama kutoa uamuzi kesho.

Tundu Lissu akiwa mahakamani

 

MAHAKAMA kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam imeahirisha shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiyi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Cahdema) Tundu Lissu mpaka kesho tarehe 23 Oktoba 2025, kwa ajili ya kutoa uamuzi mdogo… Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kesi hiyo namba 19605/25 iliendelea tena hii leo tarehe 22 Oktoba 2025, Mahakamani hapo ikiwa chini ya majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru huku wengine ni James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Uamuzi huo utatolewa kufuatia mshtakiwa Lissu kuweka pingamizi lingine kwa kuitaka Mahakama hiyo kutopokea kwa kinachoitwa ripoti ya uchunguzi kutoka kwa shaidi wa tatu wa jamhuri Samweli Kaaya.

Pingamizi hilo linakuwa la pili kwa Lissu kuliweka kwa shahidi huyo, kwa kuvikataa baadhi ya vielelezo kuingia kwenye kesi hiyo kama sehemu ya ushahidi.

Aidha mapema leo asubuhi kabla ya Mahakama kuendelea na shauri hilo, Jaji Ndunguru alisoma uamuzi mdogo wa pingamizi la awali lililohusiana na picha jongefu (video) ambapo mahakama ilikubalina na hoja za Lissu kwa kukataa kupokea kielelezo hicho.

moja ya hoja zilizokubaliwa kutoka kwa Lissu ni kwamba shahidi huyo, hakuorodheshwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kama mmoja wa wataalamu wa video.

About The Author

error: Content is protected !!