
Tundu Lissu akiwa mahakamani
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema, Tundu Lissu, leo anaweza kuanza kuandika historia yake nyingine, wakati Mahakama Kuu, itakapotolea maamuzi pingamizi lake dhidi ya serikali. Anaripoti Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).
Iwapo pingamizi la Lissu dhidi ya uhalali wa shahidi wa tatu wa serikali, Samwel Kaaya, kuwasilisha vielelezo vyake mahakamani hapo, linatajwa na watalaamu wa sheria kuwa “linabeba kesi mzima.”
Iwapo pingamizi la mwenyekiti litakubaliwa, hakuna shaka kwamba kesi mzima ya serikali, itakosa nguvu,” ameeleza mmoja wa mawakili wa Chadema kwa sharti la kutitajwa gazetini.
Kesi dhidi ya Lissu, inasikilizwa na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu – Dunstan Ndunguru, James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.
Tayari mashahidi wawili wa Jamhuri wameshakamalisha kutoa ushahidi wao.
ZINAZOFANANA
Wanafunzi 1.5 mil wa darasa la nne kuanza mtihani kesho
Mtoto wa Aboud Jumbe afariki dunia
Kesi ya Lissu yafika patamu