
KLABU ya Simba ya Tanzania, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2–1 dhidi ya Al Hilal Omdurman SC, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Alhamisi kwenye uwanja wa Meja Isamuhyo, inatarajiwa kurudiana tena katika mchezo mwingine wa kirafiki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kipute kati ya Simba na Al Hilal, kinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Jumapili ya 12 Oktoba.
Benchi la ufundi la Simba limesema, michezo hiyo ni sehemu ya maandalizi yake ya kuelekea hatua ya awali ya CAF mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba inasema, inalenga kuimarisha umoja wa kikosi, nidhamu ya kiufundi na kuondoa mapungufu yaliyojitokeza katika michezo ya awali.
Baada ya mchezo huo wa Jumapili, Simba itasafiri kuelekea Eswatini kwa ajili ya mchezo wa CAF Champions League dhidi ya Nsingizini Hotspurs, utakaochezwa katika uwanja wa Taifa Somhlolo saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
ZINAZOFANANA
Bashiri mechi za kufuzu Kombe la Dunia Jumamosi ya leo
Tusua pesa na Meridianbet kwenye mechi za kufuzu Kombe La Dunia
Meridianbet yatoa nafasi ya dhahabu mechi za kufuzu Kombe La Dunia