October 3, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Dk. Nchimbi awahimiza Liwale kuichagua CCM

Mgombea Mwenza wa CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi

 

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emmanuel Nchimbi amewaomba wananchi wa Liwale kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba 2025,siku ya Jumatano kumchagua mgombea urais wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani ili waendelee kuwatumikia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea).

Akihutubia leo Ijumaa,tarehe 3 Oktoba 2025 katika mkutano wa kampeni, uliofanyika Uwanja wa Ujenzi, Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi, amesema mambo mengi yamefanyika miaka mitano iliyopita kila sekta ikiwemo ya afya, elimu, kilimo, ufugaji na ujenzi wa barabara.

Dk. Nchimbi ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM, amenadi Ilani ya chama hicho ya mwaka 2025/2030 mbele ya umati wa wananchi akiwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo.

Pia, amesimulia nasaha alizopewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Waziri Mkuu mstaafu, Rashid Mfaume Kawawa enzi za uhai wa viongozi hao.

Liwale ndiko chimbuko la Hayati Kawawa ambaye enzi za utumishi wake aliitwa jina la ‘Simba wa Vita’ kwa sababu alikuwa haogopi kutekeleza uamuzi mzito.

About The Author

error: Content is protected !!