September 24, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Rais wa Malawi akubali kushindwa

 

RAIS wa sasa wa Malawi, Lazarus Chakwera, amekubali kushindwa katika uchaguzi mkuu nchini mwake na kuliambia taifa lake, kwamba anafanya hivyo kwa kuheshimu nia yao ya kutaka mabadiliko ya serikali. Inaripoti Mitandao ya Kijamii … (endelea).

Akihutubia taifa kabla ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa leo mchana, Rais Chakwera alisema,  anatambua matokeo ya kura za awali zinazomuonyesha mpinzani wake Peter Mutharika kuwa anaongoza kwa idadi kubwa ya kura.

Matokeo ya awali yanaonesha mpinzani wake, Rais wa zamani wa taifa hilo, Peter Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa kujizolea karibu asilimia 66 ya kura zilizohesabiwa hadi kufikia Jumanne. Chakwera alikuwa amepata 24 asilimia.

Taifa la Malawi limekumbwa na mdororo wa kiuchumi tangu mwaka 2020 alipoingia madarakani Rais Chakwera, kupitia chama chake cha Malawi Congress Party (MCP).

Amesema: “Ninajua kwamba kwa wengi wenu mliopiga kura, matokeo haya ni taswira ya nia yenu ya pamoja ya kuwa na mabadiliko ya serikali na hivyo ni sawa kukubali kushindwa kutokana na kuheshimu matakwa yenu kama raia.”

Chakwera anasema amempigia simu Mutharika kumpongeza kwa “…ushindi wake wa kihistoria.”

Alithibitisha kuwa alifika mahakamani jana kujaribu kuzuia matokeo yasitangazwe lakini akasema anakubali uamuzi wa mahakama kwamba tume ya uchaguzi lazima iendelee na kutangaza matokeo.

Chakwera pia alisema, “Wamalawi, kama mko upande wa kushindwa au kushinda, tafadhali muwe na amani.”

Mutharika ambaye aliwahi kuliongoza taifa hilo kabla ya kuondolewa na Chakwera, alijitosa kwenye mbio hizo kupitia chama cha Democratic Progressive Party (DP).

About The Author

error: Content is protected !!