September 23, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

ACT tutavunja Tume ya Uchaguzi, tutaunda upya Jeshi la Polisi

Dorothy Semu, Kiongozin wa ACT Wazalendo

 

CHAMA cha ACT Wazalendo kimetangaza Ilani yake ya Uchaguzi ambayo imejitanabaisha kwenye kuanza upya kwa kuanzisha mchakato wa Katiba mpya, kuunda upya jeshi la Polisi na kuvunja Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliyokuwepo na kuunda mpya isiyokuwa na udhibiti wa Rais wa Jamhuri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akisoma Vipaumbele vya Ilani hiyo leo tarehe 22 Septemba, Emmanuel Mvula, Mwenyikiti wa Kamati ya uandishi wa Ilani hiyo amesema kuwa utakelezaji huo utafanyika eneo chama hicho kitashika madaraka.

Amesema kuwa chama hicho kitajenga uchumi wa kujitegemea, usitegemea mikopo katika kustawisha maendeleo ya watu utakaotoa ajira milioni 12, kufufua na kujenga viwanda vipya huku asilimia 85 ya malighafi ikizalishwa ndani, kuanzisha masoko ya usiku na kuondoa vikwazo kwa mafanyabiashara wadogowadogo, tutajenga nyuma laki 5 kwa ajili ya watumishi wa umma, watu wasiojizewa na wazee.

Kipaombele cha pili cha ACT, imeahidi kutoa huduma bora zenye staha kwa jamii ikiwemo huduma ya afya isiyokuwa na matabaka na kufungamanishwa na mifuko ya hifadhi ya Jamii, kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini kwa kipindi cha miaka mitano.

Katika eneo la elimu, ACT Wazalendo imeahidi kutoa elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka elimu ya juu
na katika eneo la maji tutatoa maji bure katika kila kaya, pia eneo la nishati, itaongeza matumisi ya gesi asilia ikiwa pamoja na matumizi ya gesi kwenye gari za jamii.

Tutawawezesha kila mtanzania Bima ya afya, bima ya mazao, katika eneo la mawasiliano na uhuru wa habari , tutaondoa ukomo wa vifurushi kwenye mitandao na kupunguza gharama huduma, kutoa wifi ya bure katika maneo ya wazi na ofisi za umma.

Ndani ya Mwaka mmoja tutakamilisha mchakato wa Katiba mpya, tutavunja mara moja Tume ya Uchaguzi iliyokuwepo, tutaunda upya jeshi la Polisi kutoka chombo cha mabavu mpaka kuwa chombo cha huduma na tutafanya uchuguzi wa matukio ya utekaji.

About The Author

error: Content is protected !!