
UFARANSA imesitisha ushirikiano wa kukabiliana na ugaidi na Mali na kuamuru wafanyakazi wawili wa Ubalozi wa Mali kuondoka. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya Mali kumkamata anayedaiwa kuwa ajenti wa kijasusi wa Ufaransa mwezi Agosti. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali alikataa kutoa maoni yake.
Kusimamishwa huko kunazidisha mvutano kati ya Ufaransa na nchi hiyo ya Afrika Magharibi, baada ya Serikali ya Mali kukata uhusiano wa kijeshi na Ufaransa.
Uhusiano wa Ufaransa na nchi za eneo la Sahel umezorota katika miaka ya hivi karibuni kufuatia kupinduliwa kwa washirika wake katika nchi za Mali, Burkina Faso na Niger.
ZINAZOFANANA
Changamoto za afya barani Afrika zitatatuliwa na CDC
Chakwera adai ana ushahidi wa kura za wizi
Netanyahu acharuka Pelestina kutambuliwa