
CHAMA Tawala nchini Malawi cha Congress Party (MCP) kimesema kuwa kimegundua dosari katika kuhesabu kura katika karibu nusu ya wilaya za nchi hiyo baada ya uchaguzi wa wiki hii. Inaripoti Mitandao ya Kijamii … (endelea).
Wakati MCP wakitoa tuhuma hizo, polisi imetangaza kuwakamata maafisa wanane wa kuingiza data kwa madai ya kughushi matokeo.
Chama cha Rais Lazarus Chakwera cha Malawi Congress Party (MCP) na mpinzani wake mkuu, chama cha rais wa zamani Peter Mutharika cha Democratic Progressive Party, wote wanadai kushinda uchaguzi wa urais.
Wachunguzi wa mambo wanasema kuna kila sababu ya kuamini kuwa Chakwera amepoteza muhula wake wa pili Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) imetoa matokeo yake ya awali siku ya Ijumaa, huku matokeo kutoka kwa mabaraza matatu kati ya manne yakionyesha kwamba Mutharika mwenye umri wa miaka 85, anaongoza vyema.
ZINAZOFANANA
Uhamiaji yawang’ang’ania wageni wa Lissu
Bunge la Peru lamuondoa rais wake madarakani
Hali ya Gaza yazidi kuwa tete, Hamas haina mawasilisno na mateka