JESHI la Polisi nchini Tanzania, limeanza uchunguzi wa picha mjongeo inayosambaa katika mitandao ya kijamii, inayomuonyesha mtoto yatima aliyeiba parachichi kwa ajili ya kula na ndugu zake, akipigwa hadi kufa, mkoani Iringa. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Uchunguzi wa haraka na wa kina kuhusu picha hiyo tayari umeanza mara moja.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ndiye anayeongoza msako na ufuatiliaji wa tukio hilo. Jeshi la Polisi limesema taarifa kamili zitatolewa mara uchunguzi utakapokamilika.
Aidha, Polisi wamewashukuru wananchi wote wanaoendelea kushirikiana kwa kutoa taarifa muhimu zinazosaidia katika ufuatiliaji wa tukio hilo. Ushirikiano huo umetajwa kuwa chachu katika kufanikisha uchunguzi.
ZINAZOFANANA
Wavumbuzi Vijana wa Tanzania Waongoza Mapambano ya Tabianchi
Gwajima acharuka tena, akemea utekaji
Mahakama: Hakuna ushahidi Polepole anashikiliwa na IGP na wenzake