September 8, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Columbia Africa yaingia Tanzania kwa kuinunua IST Clinic

KAMPUNI ya Columbia Africa Healthcare Limited imetangaza ununuzi wa IST Clinic, kituo maarufu cha huduma za afya kilichopo Dar es Salaam. Kupitia ununuzi huu wa hisa kwa asilimia 100, Columbia Africa inaimarisha uwepo wake katika Ukanda wa Afrika Mashariki, ikiongeza Tanzania kwenye mtandao wake wa kliniki uliopo Nairobi, Kenya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ununuzi huu ni hatua muhimu katika mkakati wa Columbia Africa wa kupanua huduma bora, nafuu na zinazomlenga mgonjwa katika Afrika Mashariki. Baada ya mchakato wa muunganiko, IST Clinic itafanya kazi chini ya jina la Columbia Africa.

Kama sehemu ya dhamira yake ya kuboresha upatikanaji wa huduma za afya nchini Tanzania, wagonjwa wa IST Clinic wataendelea kupata huduma bila usumbufu, wakiendelea kuhudumiwa na timu ile ile ya madaktari waliowazoea, huku wakiwa sasa wanapata msaada wa utaalamu wa kimataifa kutoka Columbia Africa.

Muunganiko huu utafanya maboresho yafuatayo: Ubora wa Juu wa Huduma – kupitia utambulisho wa mifumo ya kitabibu yenye viwango vya kimataifa na kanuni za usalama kwa wagonjwa. Upatikanaji Bora wa Huduma – wigo mpana wa vipimo, mchakato wa tiba ulio rahisi, na huduma za kibingwa. Huduma Kidijitali ili Kuondokana na mfumo wa Karatasi – mfumo wa kisasa wa usimamizi wa kliniki utakaoleta uharaka wa usajili, usalama wa kumbukumbu, na urahisi wa kufanya miadi na tabibu.

Mwendelezo wa Huduma – timu iliyopo ya IST Clinic itaendelea kuwa kiungo muhimu cha utoaji huduma kwa wagonjwa. Programu Pana za Afya – upatikanaji wa huduma za kinga, programu za ustawi wa afya na utaalamu wa kimataifa.

“Tunafuraha kubwa kuipokea IST Clinic ndani ya familia ya Columbia Africa. Ununuzi huu si tu hatua ya ukuaji – bali ni ahadi ya kuleta huduma za afya za viwango vya kimataifa karibu na jamii za Tanzania, huku tukiendelea kudumisha mahusiano thabiti ambayo wagonjwa wameyajenga na madaktari wao,” alisema Dk. Sumit Prasad, Mkurugenzi Mtendaji, Columbia Africa.

Ype Smit, MD, Mwanzilishi na Mkurugenzi, aliongeza: “Kwa zaidi ya miaka 25, IST Clinic imekuwa ikitoa huduma zinazomlenga mgonjwa moja kwa moja jijini Dar es Salaam. Kujiunga na Columbia Africa kunatupa nafasi ya kuunganisha historia hii na mifumo ya kisasa ya kitabibu, teknolojia na viwango vya kimataifa vya huduma ili kuwatumikia wagonjwa wetu kwa ubora zaidi.”

Tangu kuanzishwa mwaka 1997, IST Clinic imekua na kuwa mtoaji wa huduma za afya zenye ubora wa hali ya juu jijini Dar es Salaam, ikitambulika kwa huduma za kibinafsi na endelevu. Kupitia timu yake ya madaktari, wauguzi, maabara na wafamasia, IST Clinic imetumikia vizazi vingi vya familia na kuendelea kuwa mshirika anayeaminika wa afya nchini Tanzania.

Columbia Africa, ikiwa sehemu ya makampuni ya afya ya Columbia Pacific Management, inaleta uzoefu wa miongo kadhaa katika kuendeleza hospitali na vituo vya kutoela huduma za afya barani Asia, Afrika na China. Ujio wake Tanzania unaonesha zaidi dhamira ya kujenga mifumo endelevu ya afya katika maeneo yenye ukuaji wa haraka.

About The Author

error: Content is protected !!