
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi, Innocent Bashungwa, ametoa msamaha wa kutoshtakiwa kwa wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria endapo watazisalimisha kwa hiyari ndani ya miezi miwili kuanzia tarehe 1 Septemba hadi Oktoba mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa iliyotolewa leo, tarehe 1 Septemba 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime msamaha huo utaanza kutekelezwa kuanzia leo tarehe 1 mwezi Septemba 2025 hadi tarehe 31 Oktoba 2025 baada ya tangazo la Serikali Na.537 lililotolewa tarehe 29 Agosti 2025.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote wenye silaha haramu kuhakikisha wanasalimisha ndani ya kipindi hiki cha msamaha ili kujiepusha na hatua kali za kisheria zitakazochukuliwa mara baada ya muda huo kuisha
ZINAZOFANANA
Mwendokasi Mbagala bado kuzungumkuti
Mambo matano ya Mwabukusi aliyomwambia Rais Samia
Barrick-Twiga yapongezwa kuwa kielelezo cha ubia wenye mafanikio nchini