
BODI ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Board of Tanzania -GBT), imesisitiza kuwa ni marufuku kwa watoto waliochini ya miaka kumi na nane, kushiriki michezo hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Aidha, Bodi imepiga marufuku michezo hiyo, kuendeshwa kwenye maeneo yaliyo karibu na nyumba za ibada; maeneo ya shule, karibu na maeneo ya usalama na maeneo yasiyofikia kirahisi.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, jijini Dar es Salaam, leo Jumanne, tarehe 12 Agosti 2025, Mkurugenzi wa Huduma za Bodi, Daniel ole Sumayan, alisema “…maeneo ya kuendeshea biashara ya michezo ya kubahatisha sharti yawe yamekaguliwa.”
Alisema, sekta ya michezo ya kubahatishaa imeendelea kukuwa kwa kasi nchini, kiasi ambacho mchango wa sekta hiyo kwenye uchumi wa taifa imeongezeka mara dufu.
Alisema, “Kodi ya michezo ya kubahatisha iliongezeka kutoka Sh. 131.99 bilioni kwa mwaka wa fedha 2020/21 kufikia Sh. 260.21 bilioni, mwaka 2024/2025.” Ongezeko hili, ni sawa na 97 asilimia.
Kuhusu ongezeko la ajira, Sumayan amesema, “Sekta ya michezo ya kubahatisha imetengeza ajira 30,000, imeweka uwekezaji wa Sh. 66.7 bilioni na imetoa Sh. 53.8 bilioni, zilizowekezwa katika kuendeleza michezo nchini.
Amesema: “Uwepo wa waendashaji wasio na leseni ambao hawana usajili wa GBT, hususani mashine za sloti maarufu Dibwi, hivyo husababisha mapato ya Serikali. Waendeshaji hawa wamekuwa wakiendesha biashara ya mashine hizi kiholela katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria na hivyo, kuleta usumbufu kwa jamii.
Ameongeza: “Kuruhusu ushiriki wa watoto katika sekta hii, ni kuharibu taswira ya sekta hii kwa ujumla. Bodi inaendelea kudhibiti hali hii, ikishirikiana na mamlaka nyingine za serikali pamoja na wadau mbalimbali.”
Mkutano kati ya wahariri na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
ZINAZOFANANA
Kanisa Katoliki latangaza siku ya mfungo
NBC Yaishukuru Serikali Kuzisogeza Taasisi za Fedha Karibu na Wakulima
Ahukumiwa jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka 4