
KATIKA kuelekea kwenye uteuzi wa kura za maoni nyota ya mafanikio yaanza kung’ara kwa Mtoto wa Kigogo, mkongwe na nguri wa Siasa Samwel Malecela ambaye anatajwa na wanachi wengi wa jimbo hilo wanaCCM na makada wa vyama pinzani kuwa ndiye anayefaa kuwa mbunge wa jimbo la Dodoma mjini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Wananchi katika viunga mbalimbali katika Jimbo la Dodoma ambalo kwa sasa lipo wazi baada ya kugawanywa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kugombea jimbo la Mtumba sasa anayetajwa na watu waliowengi kuwa wanaimani naye ni Samweli Mallecela ambaye amewahi kushika nafasi mbaimbali za ngazi ya juu ndani ya Chama cha Mapinduzi.
Mmoja wa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ambaye akutaka jina lake liandikwe gazetini ameeleza kuwa kama Samweli Malecel atapitishwa kwenye kura za maoni jimbo la Dodoma litakuwa limepata mtu sahihi na ndiye mtu anayefaa kuwa mbunge kwani ni mzoefu wa watu wa Dodoma na ndiye pekee anbaye anaweza kupeleka changamoto za wananchi bungeni.
“Samwel Malecela namfahamu vizuri katika medali za kisiasa na mtu ambaye ni mchapa kazi na ukiachana na hayo amekuwa kiongozi ndani ya CCM kwa ngazi za juu kwani tayari amewahi kuwa mjumbe wa NEC Taifa na mpaka sasa ni mwenyekiti wa wazazi mkoa wa Dodoma.
“Samwel tuna imani naye kweli na ukizingatia jimbo hili kutokuwa na mgombea na waliotangaza kugombea ni wapya mtu sahihi mwenye uzoefu wa siasa na mkazi halisi wa Dodoma ni yeye hivyo anastahili kabisa kuwa mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini,” amesema Kada wa Chadema.
Kwa upande wa baadhi ya akina mama wajasiliamari aliyejitambulisha kwa jina la Anna Chibago ameeleza kuwa mtu sahihi anayeweza kutatua changamoto za wananchi wa jimbo la Dodoma baada ya kugawanywa ni Samwel Malecela.
Akitaja sababu za kuwa na imani naye ameeleza kuwa jambo la kwanza ni mzoefu katika siasa na amewahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya Chama cha Mapinduzi na amekuwa mwenyekiti wa wazazi mkoa wa Dodoma lakini jambo kubwa ni pamoja na yeye kuwa mkazi halisi wa mkoa wa Dodoma tofauti na watu ambao wameonekana kuchukua fomu wakati wa uchaguzi tu.
“Waliochukua fomu wengi ni wageni hawajui changamoto za wana Dodoma hatuwajui sasa watu wa aina hiyo unawrzaje kuwa na imani nao ni vyema kumpatia mafasi ya ubunge huyu ambaye tunamjua na tuko naye muda wote,” ameeleza Anna.
Katika Jimbo la Dodoma Mjini jumla Makada wa CCM waliochukua fomu kwa ajili ya kutangaza nia ya kugombea nafasi hiyo ni makada 38.wakiwemo Mhandisi Ally, Erick Kidyala, Samwel Kisalo na wengineo.
Kwa upande wake Samwel Malecela ambaye amechukua fomu ya kutia nia kugombea nafasi ya ubunge kwa jimbo la Dodoma mjini alipotafutwa ili kuelezea kinachosemwa na wananchi kuhusu kuwa na Imani naye amesema kuwa hayo ni maoni yao.
“Hayo ni maoni yao na mtazamo wao hili jimbo kwa sasa halina mgombea na wanaogombea ni wapya,udugu mwandishi unajua aliyekuwa mbunge wa jimbo ameenda jimbo jipya la mtumba lakini zaidi ya yote vikao vya chama ndo vinatoa maamuzi na maamuzi ya chama yana heshimiwa hivyo siwezi sema chochote hapa ndugu mwandishi tusubiri maamuzi ya vikao vya chama,” ameeleza hivyo Samwel.
ZINAZOFANANA
CCM kufanya marekebisho madogo ya Katiba
Mgombea CCM agawa pikipiki kwa wajumbe
Zanzibar yatajwa kughairishwa Kamati Kuu CCM