July 24, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Orphanage Centre yafurahia ujio wa BITTECH na KMC

 

Katika mwendelezo wa kurejesha kwenye jamii, leo hii Kampuni ya Bittech kwa kushirikiana na klabu ya ligi kuu ya Tanzania KMC waliungana pamoja na kutoa msaada wa vifaa vya shule kwa watoto wa kituo hicho.

Bittech na KMC waliona kuna umuhimu mkubwa kabisa wa kufika katika kituo hicho ambacho kinapatikana Mburahati Maziwa ambapo waliweza kutoa msaada wa vifaa vya shule kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Faraja Orphanage Centre Jumatano ya leo ya mwezi wa 7.

Msafara huo uliambatana na Afisa Masoko wa Kampuni ya Bittech Bi Nancy Ingram pamoja na timu yake nzima ambao kwa pamoja walihakikisha kuwa zoezi zima la kutoa madaftari, mabegi ya shule, kalamu, penseli, na vifaa vingine vya msingi vya kujifunzia, yote hayo ni kwaajili ya kuwafanya watoto wanendelee na masomo yao kwa ari na morali mpya.

Kama inavyojulikana kuwa Elimu ni muhimu sana kwa watoto lakini pia ni haki za kila mtoto kupata elimu iliyo bora kabisa. Lakini ni ngumu mtoto huyo kupata elimu bila kuwa na vifaa ambavyo vitamuwezesha aweze kutekeleza wajibu wake wa kusoma vyema ndio maana Bittech wamekuwa mstari wa mbele kutoa msaada.

Kwa upande mwingine, mchezaji mwakilishi kutoka klabu ya KMC FC alieleza kuwa timu hiyo inathamini nafasi yake katika jamii na ina jukumu la kuwa mfano wa kuigwa ndani na nje ya uwanja akisema kuwa, “Soka ni zaidi ya mchezo. Ni sauti ya matumaini. Kama timu ya wananchi, tumeamua kuwa karibu na jamii na kugusa maisha ya wale wanaotufuatilia na kutuunga mkono.”

Walezi wa kituo cha Faraja Orphanage Centre walionesha furaha na shukrani kubwa kwa msaada huo na kwa uwepo wa wawakilishi kutoka Bittech na KMC FC, wakisema kuwa msaada huo umewatia moyo na kuwapa sababu mpya ya kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kulea watoto kwa upendo na kujitolea, “Tunapokea msaada huu kwa mikono miwili. Asanteni kwa kutuona, kutusikiliza na kutukumbuka,” alisema mmoja wa walezi wa kituo hicho.

Kupitia ushirikiano kama huu, Bittech na KMC FC wanaonyesha kuwa maendeleo ya jamii hayawezi kufanikishwa na serikali pekee, bali kwa nguvu ya pamoja kati ya sekta binafsi, michezo, na wadau wa maendeleo.

About The Author

error: Content is protected !!