
WANAKIJIJI wa Msogezo kata ya Chitete, wilaya ya Momba mkoani Songwe, wametakiwa kuacha tabia ya kunywa pombe muda wa kazi na kuipa kipaumbele katika maisha yao kwani urudisha maendeleo nyuma katika maisha yao na jamii kiujumla. Anaripoti Issa Mwadangala, Songwe … (endelea).
Akizungumza jana tarehe 14 Julai 2025 na wananchi hao Mkaguzi wa Polisi, Makubi Lagae ambaye ni Polisi kata wa kata hiyo aliwataka baadhi ya wanakiijiji hicho kuacha tabia ya kutumia muda mwingi kwenye ulevi badala ya kujishughulisha na shughuli za kimaendeleo huku akieleza kuwa pombe inapunguza uwezo wa mtu kufanya kazi kwa ufanisi, huathiri afya na huchochea migogoro ya kifamilia.
Pia Mkaguzi Lagae, alisisitiza umuhimu wa kutumia muda wa kazi kwa shughuli za kiuchumi zitakazowaletea kipato na kuboresha maisha ya familia ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kuzingatia sheria za nchi kuhusu uuzaji na unywaji wa pombe, hasa pombe za kienyeji ambazo mara nyingi zinauzwa kiholelaholela kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi.
Aidha, Mkaguzi Lagae, aliwakumbusha wazazi wajibu wao wa kuwalinda watoto dhidi ya athari za ulevi, huku akiwaomba Viongozi wa kijiji kushirikiana na Jeshi Polisi kutoa taarifa za uuzaji wa pombe haramu (gongo) na usiofuata sheria za muda uliopangwa wa kufugua na kufungwa ili hatua ziweze kuchukuliwe kwa haraka.
ZINAZOFANANA
TRA, NCAA, TANAPA na TAWA kuunda kamati ya pamoja kuongeza mapato
Wafanya usafi Kinondoni wafikiwa na Meridianbet
Biteko awaongoza washiriki 12,000 Mbio za NBC Dodoma Marathon, Mil 700 zakusanywa