June 24, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kesi dhidi ya Chadema yapigwa kalenda

John Mnyika, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema

 

KESI inayoikabili chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), kesi Na.8323/2025, imehairishwa tena hadi tarehe 10 Julai 2025, kufatia Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza shauri hilo kutokuwepo mahakamani hapo leo ambapo imeelezwa kuwa ana majukumu mengine huko Mtwara. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).

Shauri hilo linalosikilizwa kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambayo imetoa zuio kwa chama hicho kutoendelea na shughuli zake za kiutendaji mpaka shauri la msingi litakapokwisha.

Kesi hiyo ilitarajiwa kusikilizwa leo tarehe 24 Juni 2025, katika mahakama kuu baada ya kufunguliwa na aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa Chadema- Zanzibar Said Issa Mohamed na wenzake wawili dhidi ya Bodi ya wadhamini na katibu mkuu wa chama hicho

Hekima Mwasipu wakili upande wa utetezi (Chadema), amesema amepewa taarifa kuwa jaji Mwanga hakuweza kufika mahakamani kutokana na kuwa na majukumu mengine.

John Mnyika, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, amesema walitarajia hoja ya kumtaka Jaji Mwanga kujiondoa katika kesi ingesikilizwa leo aidha alieleza kuwa chama kitaendelea kuchukua hatua za ziada za kisheria ili kuhakikisha jaji huyo anaondolewa katika usikilizwaji wa kesi hiyo kwa msingi wa maslahi ya haki.

“Kwanza nieleze masikitiko yangu makubwa juu ya taarifa ya kutokuwepo kwa jaji Mwanga mahakamani, kwakuwa tarehe alipanga yeye mwenyewe na alikuwa anafahamu kuhusu ratiba, na alipanga kwa mda mrefu, shauri ambalo tarehe 10 Juni 2025 ilisikilizwa kwa uharaka …mimi nakitafsri ni kitendo cha jaji kutokutenda haki na tayali tulishaiandikia barua mahakama kuitahalifu kutokuridhishwa kwetu na mwenendo wa jaji Mwanga…”

Pia amesema wameishawasilisha maombi mahakamani ya kutaka suala la kuzuiwa chama kufanya shughuli za kisiasa lipitiwe upya na mahakama, na hivyo walitarajia ombi hilo lingepitiwa leo na kuwa wamewasilisha shauri hilo kwa hati ya dharura na walitarajia maombi yao yangeweza kusikilizwa ya kwanza na hivyo wanaamini tarehe 10 Julai shauri litakapokuja kusikilizwa tena kabla ya mambo mengine yote wanataka shauri la kumuondoa jaji Mwanga na maombi waliowasilisha ya kutaka zuio liweze kuondolewa

About The Author

error: Content is protected !!