IGP Camillius Wambura
CAMILLIUS Wambura, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania amefanya uhamisho wa makamanda watatu wa jeshi hilo. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa ya uhamisho huo imetolewa leo 17 Juni 2025 na David Misime msemaji wa Jeshi la Polisi, akiwemo ( IGP), George Katabazi kamanda wa polisi wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni siku 302 tangu alipoteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Dodoma.
Katabazi anatolewa kuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma na kuhamishiwa ofisi ya makao makuu ya upelelezi wa makosa ya jinai Dodoma.
Nafasi yake imechukuliwa na ( ACP) Galus Hyera kamishna msaidizi wa Polisi ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi kikosi cha reli.
(ACP) Matride Kuyeto kamishna msaidizi wa polisi amehamishwa kutoka kuwa mkuu wa polisi Wilaya ya Kinondoni kwenda kuwa kamanda wa polisi kikosi reli.
“Uhamisho huo ni mabadiriko ya kawaida yanayofanyika ndani ya jeshi hilo katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
ZINAZOFANANA
TRA yawataka wanachama wa SACCOS kuhamasisha ulipaji kodi
Mwanasheria wa kimataifa ataka Tanzania isifukuzwe Jumuiya ya Madola
Mwabukusi amuonya RC Chalamila, amtaja sakata la 29 Oktoba