
INSPEKTA John ambaye ni mpelelezi wa masuala ya makosa ya jinai ndani ya Jeshi la Polisi anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi Na.8606 ya uchochezi dhidi ya Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
……Inpecta John anadai kuwa alitilia shaka matamashi ya Lissu ni ya kijinai na kwamba yalikuwa yanaviashiria vya jinai.
Alipoulizwa matamshi anayoyakumbuka alijibu kuwa, “kwa kuwa hatuna Acces na Tume na hao unaona Polisi wanaingia na vibegi vya kura feki na mengine alisema majaji wote ni watu wa rais hawatatenda haki kwa sababu wanataka kupandishwa vyeo waende kwenye mahakama za rufani wapate Kameshini na kuteuliwa kwenye tume ambako huko kwenye hela.”
Maneno mengine alisema yeye anataka achaguliwe kwenye cheo fulani nchi hii na “namimi nataka nichaguliwe kwenye kacheo fulani nchi hii na nyinyi mnataka nichaguliwe kwa hali ilivyo mnadhani hili linawezekana kama haiwezekani tufanyaje mkutano wetu unasema No Reforms No Election wanasema msimamo huu unaashiria uasi ni kweli kwa sababu tutazuia uchaguzi tutaenda kukinukisha kweli kweli,” amedai.
Niliona matamshi haya yanajinai kwa sababu kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda usalama na kuweka ulinzi kwenye vituo vya kupiga kura jeshi la Polisi halihusiki wala kukusanya wala kufanya shughuli yoyote kwenye karati ya kupiga kura.
Inspekta John alidai kuwa aliona mbali kuwa uongo ukienea utaleta taharuki kwenye jamii na ni uchochezi dhidi ya Jeshi la Polisi kwa raia. “Nafahamu kuwa majaji hawaruhusi kuwa kwenye chama chochote cha siasa.”
Inspekta John alidai kuwa aliposikiliza matamshi yale aliona ni ya uongo yenye nia ya kuzua taharuki “Mheshimiwa maneno mengine ya kuzuia uchaguzi tutafanya uasi inaleta machafuko katika jamii kwani upo utaratibu mzuri wa tume uliowekwa na Katiba kwa ajili ya kupata wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi.”
Inspekta John alidai kuwa aliona matamshi hayo kwenye picha mjongeo yakitamkwa na Lissu “Mheshimiwa Tundu Lissu ni maarufu namfahamu kutokana na majukumu yake ”
Amedai kuwa baada ya kuona maudhui hayo alimjulisha mkuu wa kitengo baada ya kumwambia akamwambia akamuone Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya dar es Salaam SSP George na kwamba baada ya maagizo hayo alielekea ofisi za Kanda maalum.
Shahihi huyu alihifadhi kielelezo na kukipa namba F145 na kuandika majina yake na alama ya DM kama utambuzi.
ZINAZOFANANA
Mahakama yakubali ombi la serikali kukatisha ushahidi wa kwanza kesi ya Lissu
Kesi ya Lissu shahidi wa kwanza wa Serikali aanza kutoa ushahidi wake
Lissu apewa muda kushauriana na mawakili wake kesi ya uchochezi