
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba
SERIKALI imesema kuwa imefikia asilimia 89.6 ya malengo ya bajeti ya mwaka uliopita wa 2024/2025 ikiwa malengo ni kukusanya kiasi cha Sh. 50.29 trilioni huku ikifanikiwa kukusanya kiasi cha Sh. 45.07 trilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Hayo yamesema leo na Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha alipokuwa akiwasilisha bajeti ya fedha leo tarehe 12 Juni 2025, bungeni Dodoma.
Waziri Mwiguli amesema kuwa mapato yaliyokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), yalikuwa Sh. 26.86 trilioni, sawa na asilimia 91.3 ya lengo huku Mapato yasiyo ya kodi yanayokusanywa na Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala za Serikali, yalifikia Sh. 2.97 trilioni, sawa na asilimia 77.4 ya lengo;
Amesema kuwa mapato yanayokusanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa yalifikia Sh. 1.26 trilioni, sawa na asilimia 93.2 ya lengo na misaada na mikopo nafuu kutoka nje ya nchi iliyopokelewa ilikuwa Sh. 5.32 trilioni, sawa na asilimia 87.5 ya lengo.
Amesema kuwa Mikopo ya ndani ikijumuisha mikopo ya ndani ikijumuisha mikopo ya kulipia dhamana za Serikali zilizoiva ilifikia Sh. 6.23 trilioni, sawa na asilimia 94.1 ya lengo huku mikopo ya masharti ya kibiashara ya nje ya nchi ilifikia Sh. 2.43 trilioni, sawa na asilimia 81.3 ya lengo.
ZINAZOFANANA
Kicheko kwa watumiaji gesi za kupikia
Bajeti ya mwaka 2025/2026 trilioni 56.49
Deni la Taifa kinara kwenye matumizi