
John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi tisa kati ya kumi yaliyowasilishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuhusiana na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho- Zanzibar Saidi Issa Mohamedi na wenzake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akitoa uamuzi huo leo tarehe 10 Juni 2025, Jaji Hamidu Mwanga amesema kuwa mapingamizi hayo nahayana mashiko kisheria na kwamba kesi ya msingi inayohusu chama hicho ya kuitenga Zanzibar hususan katika mgawanyo wa rasilimali inatarajiwa kuanza kusikilizwa kuanzia tarehe 24 Juni 2025.
Awali Chadema iliwasilisha mapingamizi kumi kati ya hayo ni:- waleta maombi hawakuonesha kiwango cha fedha, waleta maombi hawakuanza kufuata taratibu za ndani ya chama kabla ya kuleta shauri mahakamani, waombaji wakati wanafungua shauri hawakuambatanisha viapo.
Waombaji kwenye shauri hilo Ahmed Rashid Khamis, Maulida Anna Komu hawana mamlaka ya kumshtaki mshtakiwa wa kwanza (Bodi ya Wadhamini wa Chadema kwakuwa wao ni miongoni mwao kwahiyo ni kama wanajishtaki wenyewe walioleta kesi hawana sababu za msingi, Kile kinachoelezwa na wadai hakioneshi kama waleta maombi wana maslahi nacho.
Waleta maombi hawana mamlaka ya kumshtaki mshtakiwa namba mbili (Katibu Mkuu wa Chadema), kesi imeletwa bila kuonyesha kifungu chochote cha kisheria, na kesi hiyo haina nyaraka sahihi.
Kesi ya msingi iliyopo mahakamani hapo kwamba Chadema, kimekuwa kikiitenga Zanzibar katika kuendesha shughuli zake ikiwemo suala la rasmali fedha. Hivyo kufungua maombi ya zuio dhidi ya chama hicho ya kufanya shughuli zote za kisiasa na kutumia mali za chama mpaka pale ambapo kesi ya msingi itakaposikilizwa,
ZINAZOFANANA
Deni la Taifa kinara kwenye matumizi
Makusanyo ya bajeti ya mwaka 2024/2025, ni Trilioni 45.7
Sheikh Ponda ajiunga rasmi ACT Wazalendo