
Leah Ulaya
LEAH Ulaya, aliyekuwa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ameshindwa uchaguzi Mkuu wa chama hicho uliofanyika jana tarehe 9 Juni 2025. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Ulaya aliyewahi kukataa uteuzi wa Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan wa tarehe 25 Januari 2023, aliyepomteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, ameshindwa uchaguzi huo na wajumbe wa CWT kumchagua Suleiman Ikomba, kutoka Temeke, jijini Dar es Salaam na kuwa Rais wa Chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Matokeo ya uchaguzi huo yametangazwa leo tarehe 10 Juni 2025. Ikomba amepata kura 608 dhidi ya kura 206 alizopata aliyekuwa Rais, Ulaya huku kura moja ikiharibika na kufanya jumla ya kura zilizopigwa kufikia 869.
Akizungumza mara baada ya kushinda kiti hicho, Ikomba amesisitiza kuwa hakutakuwepo na ukiukwaji wa misingi ya uongozi wala mizengwe ndani ya Chama kama ilivyokuwa awali
Aidha, Shaban Mwambungulu kutoka Mkoani Njombe ameshinda nafasi ya Makamu wa Rais baada ya kupata kura 236 kati ya kura 900 zilizopigwa
Joseph Misalaba kutoka Jijini Dodoma amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa CWT Taifa kwa kupata kura 742, kati ya kura 892 zilizopigwa, pia Magesa Protas Magesa kutoka Buhigwe Mkoani Kigoma, ameshinda kuwa Naibu Katibu Mkuu kwa kura 391
ZINAZOFANANA
Tundu Lissu apinga kesi yake kuahirishwa tena
Idadi ya waliofariki ajali ya Same yafikia 39
DAS Kinondoni aipongeza MONTI International kwa kuibua, kulea vipaji vya watoto