RAIS wa zamani wa Zambia Edgar Lungu amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 68, chama chake kimesema. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
“Amekuwa akipokea matibabu maalum nchini Afrika Kusini” kwa ugonjwa ambao haujatajwa, chama cha Patriotic Front kilisema kikithibitisha habari hiyo.
Lungu aliongoza Zambia kwa miaka sita kuanzia 2015, na kushindwa katika uchaguzi na Rais wa sasa Hakainde Hichilema kwa kura nyingi.
Baada ya kushindwa katika uchaguzi huo alijiondoa kwenye siasa lakini baadaye akarejea na kuonekana kuwa na nia ya kugombea tena urais
ZINAZOFANANA
Tume.yamtangaza Museven mshindi Urais Uganda
Watu 100 wameuawawa shambulio la kukamatwa Maduro
Kiongozi wa kijeshi Burkina Faso anusuruka kuuawa