
DK. Hussein Mwinyi Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar pia Rais wa Zanzibar, amempongeza Dk. Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa CCM Taifa Pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, , kwa kufanikisha kuanza kwa ujenzi wa Makao Makuu mapya ya Chama hicho. Anaripoti Joyce Ndeki, Dodoma … (endelea).
Dk. Mwinyi ametoa pongezi hizo alipokuwa akihutubia ghafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo hilo jipya, iliyofanyika Mtaa wa Salmini mkabala na Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC), jijini Dodoma, leo tarehe 28 Mei 2025.
Aidha, Mwinyi amesema kuwa Dk. Samia ameacha alama kubwa kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya Serikali, ikiwa ni kielelezo cha dhamira yake ya dhati katika kuijenga nchi na kukiimarisha Chama.
Ameongeza kuwa ataendelea kushirikiana na Rais Samia kuhakikisha ujenzi wa Makao Makuu hayo unakamilika kwa wakati, kwa hadhi na muonekano unaoendana na heshima ya Chama Cha Mapinduzi.
ZINAZOFANANA
Rais Samia aonya wanaotaka kupasua CCM
Msajili awakomalia kina Mnyika, Lema na wenzake
Mpina ashangaa watu wanatekwa Waziri bado yupo ofisini