
Eugene Kabendera
EUGENE Kabendera Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) ametangaza rasmi kujiondoa kwenye chama hicho. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Kabendera ametangaza hatua yake hiyo leo tarehe 27 Mei 2025, akidai utofauti wa kimtazamo kuhusu muelekeo wa chama ndio uliompelekea kufanya maamuzi hayo ya kujiondoa kwenyw chama hicho.
Kabendera ambeye hajasema anakwenda chama gani amesema kuwa chama hicho kimekiuka misingi na maono yaliyopelekea kukiasisi chama hicho.
Amesema uamuzi huo wa kujiondoa ni wa kimaadili unaotokana na msimamo wa kudumisha uadilifu wa kisiasa na utumishi wa kweli wa umma, na anaondoka akiwa na moyo wa shukrani kwa wote waliopambana pamoja kwa miaka 13 na kusema historia yao haiwezi kufutika ila ni wakati wa kuandika sura mpya kwa misingi ile ile ya haki, utulivu na uadilifu.
Kabendera amesema amehudumu ndani ya chama hicho kama muasisi tangu kuanzishwa kwake na kupata usajili wa muda mwezi Juni 2012 na usajili wa kudumu mwezi Julai 2013 hadi sasa miaka 13 na ameshika nyadhifa mbalimbali na katika kipindi chote amejivunia ushirikiano,kujitolea,na ushiriki wa moja kwa moja.
Pia amesema kwa sasa hajatangaza kujiunga na chama kingine na yuko wazi kuchunguza ushirikiano wa baadae wa kisisasa utakaolingana na misingi yake na maono kwa Taifa na kuwa ataendelea kushiriki kikamilifu katika maisha ya kisiasa ya nchi kwa uadilifu na dhamira ile ile inayomuongoza.
ZINAZOFANANA
Msajili awakomalia kina Mnyika, Lema na wenzake
Mpina ashangaa watu wanatekwa Waziri bado yupo ofisini
Chaumma watangaza oparesheni ya C4C, kurusha chopa nchi nzima