May 20, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Brigedia Mwakamyanda kuzikwa kesho Mbeya

 

ALLAN Jesaya Mwakamyanda, Brigedia Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), anatarajiwa kuzikwa kesho tarahe 21 Mei katika Kijiji cha Ruiwa Motomoto, mkoani Mbeya. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya Kanali Gaudentius Ilonda, Kaimu Mkuregenzi wa habari na uhusiano wa jeshi hilo, imesema kuwa taratibu za heshima za mwisho kwa Brigedia huyo zitafanyika katika Hospitali Kuu ya jeshi hilo.

Tarehe 17 Mei 2025, Mkuu Majeshi ya Ulinzi Jacob Mkunda, alitangaza kifo cha Brigedia huyo kilichotokea wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Qualitus Kigamboni jijini Dar es salaam.

Marehemu Mwakamyanda alitumikia jeshi kwa miaka 35 mwezi mmoja na siku moja,na ameacha mke na watoto.

Aliwahi kushika madaraka mbalimbali jeshini ikiwemo kamanda 121 regimenti mwaka 1999, kamanda brigedi 401 kundi la vikosi 1999 hadi 2001 na kamishna wa mipango ya jeshi katika wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa mwaka 2001 hadi alipostaafu jeshini kwa heshima tarehe 4 Julai,2004.

Kutokana na mchango wake kabila kutumikia jeshi na kulinda Taifa Raisi na amiri jeshi mkuu alimtunuku medali mbalimbali ikiwemo ya vita ya Kagera, miaka 20 ya JWTZ utumishi mrefu na uliotukuka.

About The Author

error: Content is protected !!