May 12, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Hospitali ya Mt. Joseph Peremiho yatoa nafuu mikoa ya Kusini

 

WANANCHI wa mkoa wa Ruvuma na Mikoa ya jirani ya Njombe, Lindi na Mtwara, wametakiwa kutumia Hospitali ya Peramiho ili kupata huduma mbalimbali za afya kwakuwa hospitali hiyo ina watalaamu na vifaa vya kutosha. Anaripoti Joyce Ndeki, Ruvuma … (endelea).

Ismail Ali Uss, Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa, ametoa wito huo wakati akifungua jengo la dharura (EMD) katika Hositali ya Rufaa ya Mtakatifu Joseph Peramiho, iliyopo katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

“Kwakweli Mwenge wa Uhuru wa Kitaifa umepita na kukagua katika hospitali yetu ya Rufaa ya Mtakatifu Joseph hapa Peramiho, mradi huu umesimamiwa vizuri, una ubora, wananchi mjitokeze kupata huduma katika hospitali hii ikiwemo wa mikoa jirani,” amesema Uss

Kwa upande wake Jenista Mhagama Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho, amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi inaendeea kushirikiana kwa kuwa ni washirika na sio washindani.

“Katika kuonesha ushirikiano huo, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Samia Suluhu Hassan inalipa mishahara ya watumishi 295 kwenye hospitali hii ya misheni ya Mtakatifu Joseph hapa Peramiho,” amesema Waziri Mhagama.

Mwenge wa Uhuru upo mkoani Ruvuma leo ikiwa ni siku ya pili (2) ambapo unakimbizwa katika Halmashauri ya Songea vijijini na kesho utakimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa lengo la kukagua, kufungua na kuweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali.

About The Author

error: Content is protected !!