
TAASISI ya Dk. Godwin Mollel kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation zimetoa huduma ya bure ya matibabu ya macho kwa wananchi zaidi ya 3,000 katika Hospitali ya Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro. Anaripoti Joyce Ndeki, Kilimanjaro …(endelea).
Akizungumza wakati wa kambi hiyo ya matibabu, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel amesema huduma hizo zinajumuisha upasuaji wa macho, utoaji wa dawa na miwani kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa jamii, hususan kwa wenye uhitaji.
Pia amewataka wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hizo zinazoendelea kutolewa bure.
“Huduma hii ni sehemu ya ushirikiano baina ya Serikali na sekta binafsi ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya bila vikwazo vya kiuchumi ambapo taasisi ya Dk. Mollel na Mo Dewji zitagharamia matibabu yote bure kwa wananchi,” amesema Dk. Mollel.
Dk. Mollel ameongeza kuwa, taasisi hizo zimeweka kambi hiyo ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa juhudi zao za kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi wote nchini
ZINAZOFANANA
Serikali kukarabati vituo konhwe vya huduma ya afya
RHMT na CHMT sikilizeni kesro, maoni kutoka kwa wananchi – Dk. Mfaume
Dar yatakiwa kujenga vituo vya Afya jwa ghorofa