May 12, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Trump asema hatawania urais kwa muhula wa tatu

Rais wa Marekani, Donald Trump

RAIS wa Marekani, Donald Trump amekanusha madai yanayodai anafikiria kugombea muhula wa tatu wa urais, hatua ambayo wataalamu wanakubali kuwa ni marufuku kwa mujibu wa Katiba ya Marekani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

“Nitakuwa rais wa miaka minane, nitakuwa rais awamu mbili. Siku zote nilifikiri hilo lilikuwa muhimu,” Trump alikiambia kipindi cha Meet the Press cha NBC na Kristen Welker katika mahojiano yaliyopeperushwa Jumapili.

Trump, mwenye umri wa miaka 78, alisema hapo awali kwamba “hakuwa na mzaha” kuhusu kutaka kuhudumu muhula wa tatu, au hata wa nne kama rais wa Marekani.

Baadaye alisema taarifa zake zilikusudiwa kuviudhi “vyombo vya habari bandia.”

Kampuni yake, The Trump Organization, imekuwa ikiuza kofia za “Trump 2028” na hivyo kuchochea uvumi kwamba anaweza kutaka kusalia madarakani baada ya muhula wake wa pili kukamilika Januari 2029.

Katika mahojiano hayo, yaliyorekodiwa kutoka kwenye makazi yake huko Florida siku ya Ijumaa, Trump alisema kuwa amekuwa na “maombi” mengi kutoka kwa watu wanaomtaka afikirie kutaka kusalia ofisini.

“Watu wengi wanataka nifanye,” Trump alisema, siku chache baada ya kusherehekea siku zake 100 za kwanza za muhula wake wa pili. “Ni kitu ambacho, kwa ufahamu wangu, huruhusiwi kukifanya. Sijui kama hiyo ni ya kikatiba ambayo hawakuruhusu kulifanya au kitu kingine chochote,” Trump alisema.

Aliongeza kuwa “kuna watu wengi wanaouza kofia ya 2028,” “Lakini hili si jambo ninalotazamia kufanya,” alisema, akiendelea kuorodhesha Warepublican ambao wanaweza kuchukua nafasi yake, akiwemo Makamu wa Rais JD Vance na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubi.

Marekebisho ya 22 ya Katiba yanasema kwamba “hakuna mtu atakayechaguliwa kushika wadhifa wa Rais zaidi ya mara mbili.”

About The Author

error: Content is protected !!