
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kwa Kamanda wake, Muliro Jumanne limesema limemkamata mtu mmoja kwa tuhuma za kumshambulia Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Padri Charles Kitima jana. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa jana tarehe 30 April 2025 saa nne usiku maeneo ya Baraza la Maaskofu Kurasini Dar e Salaam, ilipokelewa taarifa ya kujeruhiwa kwa Padri Kitima ambapo tangu saa tatu asubuhi viongozi wa dini mbalimbali walikuwa katika kikao.
Imeelezwa kuwa baada ya kikao kwisha saa moja jioni, Padri huyo alikwenda kantini alikokaa hadi saa nne na robo usiku ambapo aliponyanyuka kwenda maliwatoni pembeni ya kantini hiyo kushambuliwa kichwani na watu wawili ambao walitumia kitu butu kumshambulia.
Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa Padri huyo aliwaishwa Hospitali na anaendelea vizuri kwa sasa ambapo tayari mtu mmoja kati ya wawili hao amekamatwa na kutajwa kuwa Rauli Mahabi Haraja, Mkazi wa Kurasini ambaye anashikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo “uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua kali na za haraka zichukuliwe kwa Wahusika”
ZINAZOFANANA
Luhemeja ataka Afrika yenye kukabili mabadiliko ya tabianchi
John Mrema avuliwa uanachama Chadema
Mwanza mbioni kuzalisha vyanzo vipya vikubwa vya kodi