
Rais wa Rwanda, Paul Kagame
RWANDA imewashikilia maafisa watatu wakuu wa Bodi ya Migodi, Petroli na Gesi, nchini humo pamoja na wafanyabiashara wanne wanaoshukiwa kuhusika na rushwa na matumizi mabaya ya mamlaka. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Ofisi hiyo ya upelelezi, imesema watatu hao ni Augustin Rwomushana, John Kanyangira na Richard Niyongabo wanazuiliwa katika mji mkuu wa Kigali, bila kutaja ni lini walikamatwa.
Taarifa ya ofisi hiyo ya uchunguzi imeongeza kuwa maafisa hao watatu walikamatwa pamoja na wafanyabiashara wanne wanaoshukiwa kuhusika katika uhalifu unaohusisha rushwa, matumizi mabaya ya mamlaka kwa kutumia ofisi zao kwa maslahi yao binafsi, kujilimbikizia mali kinyume cha sheria pamoja na utakatishaji fedha .
Haya yanajiri baada ya Umoja wa Ulaya mwezi Machi kuwawekea vikwazo viongozi wa bodi hiyo, kufuatia hatua ya Rwanda ya kuwaunga mkono waasi wa M23 huko nchini DR Congo ili kujipatia madini muhimu.
Haijabainika wazi iwapo maafisa hao wanahusishwa na biashara haramu ya madini kutoka eneo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako Rwanda inashutumiwa kuwaunga mkono wapiganaji wanaoipinga serikali ya Congo kufanya ulanguzi wa madini hayo.
ZINAZOFANANA
Matumizi ya kijeshi yaongezeka duniani kwa kiwango kikubwa
Makardinari kuchagua Papa mpya
Kesi ya Israel kuanza kusikilizwa