
Kapteni Ibrahim Traoré
KATIKA hali isiyo ya kawaida, jina la Kapteni Ibrahim Traoré, kiongozi kijana wa Burkina Faso anayejitambulisha kama mpigania haki za Waafrika, limeingia katika vichwa vya habari vya dunia, si kwa mapinduzi aliyoyafanya tu, bali kwa kile kinachotajwa kuwa ni shinikizo kutoka kwa Marekani kutaka akamatwe. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Tuhuma hizi hazijatolewa na mtu wa kawaida, bali ni kutoka kwa Jenerali wa nyota nne wa Marekani, Michael E. Langley, ambaye ni Kamanda wa Kikosi cha Marekani cha Afrika kinachoitwa United States Africa Command (AFRICOM).
Katika kikao rasmi cha Baraza la Seneti la Marekani wiki hii, Langley aliitwa kutoa tathmini kuhusu hali ya usalama barani Afrika. Katika maelezo yake, alimtaja wazi Kapteni Traoré, akisema kwamba anatumia dhahabu ya taifa lake “kujilinda binafsi” badala ya kuwalinda wananchi, na akaongeza kuwa kuna haja ya kumchukulia hatua kali za kimataifa, akisema:
“Tunapendekeza hatua mahususi, vikwazo vya kifedha, ushirikiano wa kimataifa, na ikiwa itahitajika, Traoré azuiliwe ili kulinda maslahi ya kikanda na kimataifa.”
ZINAZOFANANA
Shirika la Amnesty kuchunguza matukio ya wafuasi wa Chadema kupigwa Kisutu
Papa Francis kujifunza upya kuongea
Trump: Uchumi wa Marekani upo katika kipindi cha mpito