
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa amewataka watanzania kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi kama sehemu ya kuhimarisha afya zao pamoja na kuchangia mambo ya kimaeendeleo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati wa akizungumza na wabunge,wadau wa Maendeleo na watanzania wa rika mbalimbali kwenye hitimisho la Bunge Marathon lililokuwa likilenga kuchangisha zaidi ya shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kujenga shule ya wavulana ya bweni ya kidato cha tano na sita itakayojengwa kata ya Kikombo Jijini Dodoma.
Majaliwa amesema kuwa Bunge kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na wananchi kwa ujumla wake wamefanya jambo hilo kwa lengo la kuwahamasisha watanzania kwa kushirikiana na Bunge kujenga shule ya mfano ya bweni ya wavulana ambayo itakuwa na huduma muhimu za kutaaluma na kuwafanya wanafunzi watakaojiunga na shule hiyo kufurahia masomo watakayo patiwa shuleni hapo.
“Shule itakuwa na maabara 4 za kisasa, itakuwa na mabweni ya uwezo wa kulaza wanafunzi 300,maktaba kubwa na ya kisasa,nyumba za walimu pamoja na viwanja vya michezo.
“Shule hii inajengwa baada ya Bunge kujenga shule ya kisasa ya mfano ya wasichana ambayo kwa sasa matokeo yake yanaonekana na hii ni kuonesha kuwa serikaki inawajali watoto wa kile na kiume”ameelezaa Majaliwa.
Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa ujenzi wa Shule hiyo ni mwendelezo wa ujenzi wa shule za kike za watoto wenye mahitaji maalumu pamoja na uboreshaji na uandaaji wa mfumo wa TEHAMA na kuzifanya kutoa masomo ya Amari.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Tanzania Dk.Tullia Akson muda mfupi kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasm na kufanikiwa kukimbia umbali wa Killometa 5,Dk.Tulia amesema Bunge linaendesha michango kwa ajili ya kuwekeza katika elimu kama sehemu ya alama ya Bunge.
“Sisi wabunge tunatambua umuhimu wa watoto wa kike na kiume hivyo sasa tunahitaji kujenga shule ya kisasa ya wavulana ambayo itakuwa na ubora unaokubalika kitaaluma”amesema Spika.
ZINAZOFANANA
Jumamosi ya kuchukua kitita cha maana ni leo
Waziri Masauni aelezea mafanikio ya Muungano
Ofisi ya Msajili Hazina yaendesha mafunzo kwa kamati za bunge