
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kinaendelea kufuatilia kwa karibu juu ya tuhuma zinazosambazwa mitandaoni kuhusu madai ya kupigwa kwa Mratibu wa Uenezi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), Sigrada Mligo. Anaripoti. Mwandishi Wetu. Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 31 Machi 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho, Brenda Rupia, ikieleza kuwa Chama hicho kinafanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli wa jambo hilo na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na Miongozo yake.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo CHADEMA inafuatilia kwa makini njama za Chama cha Mapinduzi (CCM) za kutumia tukio hili kwa manufaa yao binafsi.
“Tunatoa wito kwa Sigrada Mligo kuwa makini na mahusiano yake na (CCM) ili kuepuka kutumiwa kwa malengo yasiyo na nia njema, ambayo yanaweza kuathiri si tu hadhi ya Chama bali na ya kwake pia kama kiongozi na usalama wake binafsi,” imesema taarifa hiyo.
Pia, taarifa hiyo imeeleza kuwa chama hicho kinaendelea kufuatilia kwa karibu kila hatua inayochukuliwa kwa kushirikiana na vyombo husika vya ndani na nje ya chama, na baadae watatowa kauli rasmi kuhusu suala hilo kadri itakavyofaa.
ZINAZOFANANA
Sheikh Ponda: Mifumo ya uchaguzi irekebishwe
Wassira ataja Chanzo cha Deni la Sh. 97 Trilioni.
Bawacha Nyasa: Siglada ni mtovu wa nidhamu