March 31, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Walimu 1,585 wapatiwa mafunzo ya Tehama na UCSAF

 

KWA kipindi cha miaka 4 ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassani, walimu wapatao 1585 wamepatiwa mafunzo juu umuhimu wa matumizi ya TEHAMA. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Peter Mwasalyanda alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka 4 ya uongozi wa serikali iliyopo madarakani katika Ofisi za Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dodoma.

Mhandisi Mwasalyanda amesema kuwa kitendo cha kuwapatia elimu ya TEHAMA walimu hao ni hatua kubwa ya kuwawezeshe kutenda kazi zao kwa kujiamini na kwa uzoefu na kazi zao.

Ameeleza kuwa elimu hiyo kwa walimu itawawezesha pia kuvielewa vifaa vya tehama hata pale vinaposumbua wasipate usumbufu wa kuwatafuta mafundi kwa mambo ambayo wanaweza kuyafanya wenyewe na kuwafundisha wanafunzi kwa uelewa zaidi.

Aidha amesema kuwa kutokana nanumuhimu wa elimu ya TEHAMA, UCSAF imepeleka vifaa katika shule zenye uhitaji maalumu vyenye gharama ya Sh. 1.8 bilioni.

Akizungumzia kuhusu uboreshaji wa mawasiliano amesema kuwa jumla ya minara 758 imejengwa na inatarajiwa kufikia Mei 12 mwaka huu itakuwa imekamilika.

Amesema kwa kipindi cha miaka 4 minara 758 imejengwa na kati ya hiyo minara 430 tayari inatoa huduma.

Aidha ameeleza kuwa minara hiyo itawahudumia watanzania milioni 8.5 ambapo serikali imewezesharuzuku ya shilingi bilioni 126.

About The Author

error: Content is protected !!