
UONGOZI wake Rais Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha miaka 4 umeiwezesha Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kufikia mafanikio takribani 12 jambo ambalo ni la kihistoria tangu kuwepo kwa Taasisi hiyo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Hayo yameelezwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST Nokta Banteze alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya Taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka 4 ya Rais aliyepo Madarakani katika Ukumbi wa Habari -MAELEZO Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa kutokana na tafiti zinazofanywa na GST, zimewezesha kuchangia sehemu kubwa ya mnyororo wa uchumi kwa kupelekea migodi mingi (midogo, ya kati na mikubwa) kuanzishwa.
Akiendelea kuelezea amesema kuwa ukiacha jukumu la utafiti wa madini nchini, GST ina maabara ya kisasa inayotoa huduma za uchunguzi wa madini kwenye sampuli za miamba, udongo, maji na mimea.
Katika maelezo yake amesema maabara hoyo ni kubwa na ya kipekee ya Serikali na inaendeshwa kwa kuzingatia miongozo ya kimataifa (accreditated laboratory).
Akiachilia mbali maelezo ya kuwepo kwa GST ameweka wazi mafanikio ya taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka 4 na kueleza kuwa katika kipindi cha miaka minne (2021 2025) cha Serikali ya Awamu ya Sita, GST imeshuhudia mafanikio lukuki.
Akiyataja mafanikio hayo amesema ni pamoja na kuongezeka kwa Makusanyo ya ndani kutoka wastani wa shilingi 1,251,428,472.91 mwaka 2021 hadi shilingi 2,394,211,348 mwaka 2023/2024, sawa na ongezeko la asilimia 91.32.
Amesema ongezeko hilo limepatikana kupitia mageuzi na maboresho mbalimbali ya kiutendaji yaliyofanyika katika kipindi husika ambayo yaliongeza ubora wa huduma zitolewazo na GST;
Aidha amesema Kuongezeka kwa idadi ya sampuli zinazochunguzwa kutoka wastani wa sampuli 19,184 mwaka 2021 hadi sampuli 25,793 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 34.45.
“Ongezeko hili limetokana na maboresho makubwa ya maabara yaliyofanyika hasa katika ununuzi wa vifaa na mashine za kisasa za uchunguzi wa sampuli;
“Kuongezeka kwa bajeti ya Taasisi kutoka wastani wa shilingi bilioni 10 mwaka 2021/2022 hadi bilioni 110 mwaka 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 1,000 kwa ajili ya kukamilisha majukumu mbalimbali ya Taasisi ikiwemo miradi ya maendeleo.
“GST ilikamilisha ugani wa jiolojia kwa lengo la kubaini miamba na madini yanayopatikana kwenye QDS 278 na 290 zilizopo Hifadhi ya Taifa ya Mwalimu Nyerere na Pori la Akiba la Selous katika sehemu ya Mikoa wa Lindi na Ruvuma), QDS mbili (2) mpya ambazo ni QDS 203 na 204) katika sehemu ya Mkoa wa Pwani na sehemu ndogo ya Mkoa wa Dar es salaam.
“Matokeo ya awali ya utafiti yanaonesha uwepo wa mchanga wa ujenzi, madini ya dhahabu na urani kwenye QDS 278 na 290; na uwepo wa madini ya kaolin, chokaa, udongo mfinyanzi, silica sand, madini tembo (heavy mineral sands) na metali adimu (rare earth elements) kwenye QDS 203 na 204,(note, QDS ni quarter degree sheet eneo lenye ukubwa wa kilometer 54 kwa 54).
“Matumizi ya madini adimu kukamilisha ugani wa jiolojia na jiokemia kwa lengo la kubainisha mikondo ya madini kwa QDS 125 (iliyopo katika sehemu ya Wilaya za Kiteto, Chemba na Chamwino) na QDS 126 (iliyopo katika sehemu ya Wilayani ya Kiteto). Ugani huo ulibaini uwepo wa madini ya chokaa;
“GST kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikamilisha utafiti na uchoraji wa ramani ya jiolojia ya visiwa vya Zanzibar (Unguja na Pemba); ikumbukwe kuwa visiwa vya Zanzibar havijawai kufanyiwa utafiti huo wa jiolojia.
“Matokeo ya utafiti huo yamebaini uwepo wa miamba ya chokaa yenye ubora wa kutengeneza saruji, madini tembo (heavy mineral sands), madini ya silica, strontium, vyanzo vya maji ardhi, maeneo yenye vivutio vya utalii wa jiolojia na maeneo hatarishi kwa majanga ya asili ya jiolojia,” ameeleza Banteze.
ZINAZOFANANA
Waziri Biteko ahimiza mabadiliko Jeshi la Magereza
Serikali: Faida itokanayo na uwekezaji ifikie zaidi ya asilimia 10
Shirika la Posta limezalisha hasara ya 23.63 bilioni kwa mwaka – CAG Kichere