
Katibu wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na mgombea wa urais, Dk. Wilbrod Slaa amerejea rasmi ndani ya chama hicho hii leo baadaya miaka 10 na kupokelewa na Mwenyekiti Taifa Tundu Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).
Slaa amerejea Chadema leo tarehe 23 Machi 2025, jijini Mbeya wakati wa uzinduzi wa kampeni ya No Reforms, No Election iliyofanyika kwenye uwanja wa Ruanda Nzovwe.
Katika hotuba yake mara baada ya kurejea Dk. Slaa alitanguliza kuomba msamaha, kwa wafuasi na wanachama wa Chadema ambao walikwaruzana wakati mara ya mwisho akiondoka ndani ya chama hicho, kwenye vuguvugu la uchaguzi mkuu mwaka 2015.
“Mimi naomba radhi kwa sababu kama kuna mkwaruzano na tukitaka kurudiana tunaomba msamaha, mimi niombe msamaha hadharani, niombe radhi kwa ndugu zangu wa makao makuu na wanachadema wote Duniani,” alisema Slaa
Mwanasiasa huyo anakuwa mtu wa kwanza kurejea Chadema, toka ulipoingia madarakani uongozi mpya chini ya Tundu Lissu, huku idadi kubwa ya waliokuwa wanachama wa chama hicho zamani ambao walitoka, inasemekana watarejea tena hivi karibuni.
Kampeni hiyo ambayo inafanyika kupitia mikutano ya hadhara, itafanyika kwa siku 40 katika kanda zao mbalimbali, ikiwa le oni ufunguzi kwenye kanda ya Nyassa, ikiwa ina jumuisha mikoa ya Mbeya, Iringa na Tunduma.
ZINAZOFANANA
Hatua za msajili analenga kuinyamazisha ajenda ya Chadema
Askofu Mwamalanga akemea vikali kauli ya Makala
Tundu Lissu atoa sababu za kutaka mabadiliko ya Uchaguzi