
Amos Makala
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepanga kuwafungulia kesi Mahakamani, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Amos Makalla kuhusu kauli aliyoitoa ya kuwa Chadema wanatumia michango ya Tone Tone, ili kuingiza virusi vya ugonjwa wa Ebora na M-POX nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).
Kauli ya Chadema kuhusu kesi hiyo, imetolewa na Makamu Mwenyeti Bara John Heche, ambapo alimuomba Mwenyekiti wake Tundu Lissu, kuwataka wanasheria wao wa chama kufungua kesi hiyo dhidi ya Makalla na gazeti la Habari Leo.
“Mwenyekiti wewe ni Mwanasheria, nina kuomba uwaagize wanasheria wetu wawafungulie kesi hawa watu, tunataka watuambie ni wapi virusi vinauzwa, vinauzwa shilingi ngapi na Chadema imenunua kwa bei gani,” alisema Heche.
Kauli hiyo ya Makalla haikuishia kushambuliwa tu Heche lakini pia ilimuibua, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Amani Golugwa ambaye alisema kuwa kauli hiyo ni ya hovyo na hivyo Makalla au chama chake wanapaswa kuomba radhi.
Makalla alitoa kauli hiyo jana tarehe 22 Machi 2025, mkoani Simiyu katika maadhimisho ya miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Alisema kuwa Chadema kinakusanya fedha kwa kisingizio cha kuandaa umma kupinga uchaguzi kupitia kampeni inayojulikana kwa jina la Tone Tone, lakini lengo ni kununua virusi vya Ebola na Mpox ili viingizwe nchini na kuvuruga uchaguzi wa mwaka huu.
ZINAZOFANANA
GF Automobile, NaCoNGO zasaini makubaliano ya kimkakati
Hatua za msajili analenga kuinyamazisha ajenda ya Chadema
WMA yajivunia kuongezeka kwa ajira nchini