March 23, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wanafunzi wahimizwa kulinda miundombinu ya shule

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa

 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amepongeza Serikali kujenga miundombinu bora katika shule za sayansi za wasichana, ahimiza wanafunzi kulinda miundombinu iliyowekwa ili iwe na tija. Anaripoti Apaikunda Mosha, Njombe … (endelea).

Mapema leo tarehe 22 Machi, 2025 wakati wa ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo Njombe, Majaliwa ametembelea Shule ya Sekondari ya Mkoa ya Wasichana ya katika mkoa huo Wilaya ya Wanging’ombe,

Ametoa wito kwa wanafunzi wa shule zote nchini kuwa na ushirikiano mzuri baina yao wenyewe, pia kuwajali na kuwasaidia wanafunzi wenzao wenye mahitaji maalum ili nao waweze kutimiza ndoto zao.

Pia kutokana na kuridhishwa na ujenzi na mandhari ya shule hiyo na kuvutiwa na mifumo ya TEHAMA ambayo imewekwa Majaliwa ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa shule za wasichana zenye viwango mikoa yote hapa nchini.

“Nimevutiwa na mindombinu ya TEHAMA iliyopo katika shule hii, wanafunzi mhakikishe mnaitunza ili iwe na tija na kutimiza malengo yenu ya kujisomea,” amesema Majaliwa. 

Naye, Naibu Waziri OR-TAMISEMI na Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe Festo Dugange, amemshukuru Rais Samia kwa kuwezesha upatikanaji wa shule hiyo sambamba na miradi mingine mingi ya maendeleo ikiwemo vituo vya afya, huduma za maji na miundombinu ya barabara.

Aidha, Mradi wa ujenzi wa Shule hiyo umegharimu zaidi ya Sh. 4 Bilioni, shule hiyo ina jumla ya vyumba vya madarasa 22, mabweni 9, bwalo, jiko pamoja na miundombinu mingineyo, na kwa sasa tayari imedahili wanafunzi 460 wa michepuo mbalimbali ya masomo.

About The Author

error: Content is protected !!