
PAPA Francis
PAPA Francis (88) anaendelea kurejesha nguvu zake polepole hospitalini lakini analazimika “kujifunza tena kuzungumza” baada ya matumizi ya muda mrefu ya tiba ya oksijeni yenye mtiririko mkubwa, Kardinali Victor Manuel Fernandez amesema. Inaripoti Mashirika ya Habari ya Kimataifa … (endelea).
Kardinali huyo, ambaye ni mkuu wa ofisi ya mafundisho ya imani ya Vatican, alikanusha uvumi kwamba Papa angejiuzulu na kusema kuwa anarejea katika hali yake ya kawaida.
“Papa yuko vizuri sana, lakini oksijeni yenye mtiririko mkubwa hufanya koo kukauka sana. Anahitaji kujifunza tena jinsi ya kuzungumza, lakini hali yake ya jumla ya mwili iko kama ilivyokuwa hapo awali,”* Fernandez alisema wakati wa uzinduzi wa kitabu kipya cha Papa kuhusu ushairi.
ZINAZOFANANA
Mchengerwa amuonya vikali Chalamila
Chadema kuanza kuwasha moto Jumapili hii
Wassira amchongea Mo Dewji kwa serikali kwa kutelekeza mashamba ya Rungwe