
Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mwangwala
MKUU wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mwangwala, amesema kuwa endapo wananchi wataelewa umuhimu kulipa kodi na athari za biashara za magendo nchi itakuwa salama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).
Hayo ameyasema wakati wa ziara ya Maofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), idara ya forodha. DC Mwangwala alisema kuwa amewapa baraka maofisa hao kwenda kuwapa elimu wananchi.
“Elimu ni muhimu hatuzungumzii tu magendo , tunazungumzia mtu anaweza kuingiza silaha , mtu anaweza kuingia sumu ambayo itaathiti nchi yetu mtu anaweza wahamiaji harama ambao huwezi kuelewa ni maharamia au magaidi kwa hiyo tunapozungumzia kuangalia mipaka yetu hatuzungumzi kwenye muktadha wa kodi tu , tunazungumzia muktadha wa kiusalama, mapato , tunazungumzia mambo ambayo mwananchi akiyaelewa utakuwa msaada mkubwa kwa nchi yetu,” alisema DC Mwangwala.
“Nendeni mtusaidie elimisheni watu waweze kuelewa tunakuwa tumeisaidia nchi yetu kwa kiasi kikubwa,” alisema DC Mwangwala.
DC Mwangwala, alipendekeza kuwa elimu hiyo itolewe kwa Watendaji na wenyeviti wa vitongoji ambao hawa wako karibu na wananchi
Amesema kuwa endapo mapato yakakusanywa vizuri basi nchi itapata maendeleo. “Mnafanya hivyo lengo letu kuisaidia nchi , tunakuwa tuwasaidia Watanzania na tunakuwa tumemsaidia Rais wetu,” alisema DC Mwangwala.
Amesema kuwa endapo wananchi wakaelewa umuhimu wa kodi na usimamizi ukawa nzuri basi nchi itajisimamia .
“Hakuna mtu atakayeweza kutunyanyasa kwa sababu tunakuwa na uwezo wa kujiendesha wenyewe mapato ya ndani tunaambiwa sasa yanafikia asilimia 70, kwa hiyo kama tumefika hatua hiyo tunaweza kujiendesha wenyewe,” alisema DC Mwangwala.
Ametoa wito kwa maofisa wa TRA kufanya shughuli zao kwa uadilifu.
Ameitaja changamoto ya maeneo ya mipaka kutorasimishwa kwenye forodha kwa kuwa kuna njia zinazotumika kutoka ambapo haziwa mawakala wa forodha.
ZINAZOFANANA
Cat Purry kasino mtandaoni inayokupa malipo makubwa
Vodacom, dLab wawezesha wasichana kupitia programu ya CODE LIKE A GIRL
Serengeti yatambuliwa Tuzo za Rising Woman kwa kukuza usawa wa kijinsia