
ASKOFU Msaidizi wa jimbo kuu la Dar es Salaam, Stephano Lameck Musomba, O.S.A, ameteuliwa kuwa, Askofu wa kwanza wa jimbo jipya la Bagamoyo linaloanzishwa leo tarehe 07 Machi, 2025. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa hii imetolewa leo na BARAZA la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC) leo tarehe 7 Machi 2025 imeeleza kuwa uteuzi huo umefanywa na Baba Mtakatifu Francisco.
Aidha taarifa hiyo imeeleza historia yake kwa ufupi kuwa “Mhashamu Askofu Musomba alizaliwa tarehe 25 Septemba 1969 Malonji jimboni Mbeya”.
“Baada ya masomo yake ya upadre, alipewa daraja takatifu la upadre tarehe 24 Julai 2003 na kuhudumu katika nafasi mbalimbali za utume shirikani, jimboni Dar es Salaam na Morogoro,” imeeleza.
Pia imeelezwa kuwa hadi uteuzi wake Mhashamu Askofu Musomba bado alikuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam tangu mwaka 2021.
Aidha, katika kutekeleza majukumu yake BARAZA na uongozi wanamwombea afya njema ya roho na mwili katika utume wake huo mpya.
ZINAZOFANANA
Serengeti yatambuliwa Tuzo za Rising Woman kwa kukuza usawa wa kijinsia
ALAT kujadili ripoti ya CAG
NBC yaandaa hafla ya futari Zanzibar, yajivunia ongezeko la wateja