
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Bumbuli kutumia fursa ya Jengo jipya la Halmshashauri kupata huduma kwa urahisi . Anaripoti Apaikunda Mosha. Tanga … (endelea).
Akizungumza baada ya kufanya uzinduzi wa jengo hilo Jumatatu, 24Februari 2025, Rais Samia amepongeza jitihada na nguvu kubwa ilizofanyika kwa wote walioshiriki katika kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ikiwa ni sehemu ya miradi ya kimaendeleo nchini.
Amewashukuru wakandarasi, washauri, na wafanyakazi wa Halmashauri kwa juhudi zao katika kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa ubora, na kuwaeleza kuwa kazi yao ni mfano mzuri wa ushirikiano wa kiutendaji.
Rais Samia amesema kuwa jengo hilo limejengwa kuhakikisha watumishi wa Halmashauri wanafanya kazi katika mazingira bora na wananchi wanapata huduma kwa kuwafikia kiurahisi.
Hata hivyo, kukamilika kwa jengo hilo kutapelekea watumishi wote kuwa eneo hilo kutoa huduma na kuboresha huduma kwa wananchi, pamoja na kutoa fursa kwa watumishi kufanya kazi zao kwa ufanisi.
“Jengo hili ni la wananchi wa Bumbuli. Mazingira mazuri ya kazi na huduma zote zitatolewa hapa mara baada ya kuletwa kwa watumishi ili watoe huduma zote hapa, na naomba mlitumie kwa manufaa yenu,” amesema Rais Samia.
Aidha, Rais Samia ameeleza furaha yake kwa kupokelewa vizuri na wananchi wa Bumbuli wakiongozwa na Mbunge wao Januari Makamba, pia ameshukuru kwa kuona mabango ya upendo kutoka kwa wananchi ambayo yanayosomeka: “Tunakupenda sana Mama.”
ZINAZOFANANA
Benki ya Exim yaingia mkataba wa miaka mitatu na ZATI
Makamba amhakikishia Rais Samia kushinda kwa kishindo Lushoto
TPA yataja miradi 10 ya kimkakati