
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Erick Shigongo
MBUNGE wa Jimbo la Buchosa Erick Shigongo amesema Afrika ni Bara tajiri hivyo umasikini uliopo, ni changamoto ya uwezo wa kutumia rasilimali ambazo Mungu ametupa na kuzibadilisha ziwe fedha ili zilete maendeleo. Anaripoti Apaikunda Mosha. Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza leo Februari 22 na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la pato la nchini kwa sasa.
Amesema GDP ndani ya miaka mitatu iliyopita ilikuwa inakadiriwa kuwa Dolla za kimarekani bilioni 67 mpaka sasa hivi limeongezaka na kufikia bilioni 85.
Ameipongeza Serikali kwa jitihada kubwa za kuinua uchumi wa nchi yetu kufikia asilimia 5 baada ya kushuka kwake kutoka asilimia 6 mpaka 2.5 kutokana na changamoto na maafa makubwa yaliyotokea Dunia nzima kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Ameeleza namna ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan amesitisha misaada ili tuweze kutumia utajiri wetu kupata maendeleo, sambamba na hilo ameanisha mapato ya nchi kupitia sekta mbalimbali kama utalii, madini na kilimo yalivyoongezeka kwanzia mwaka 2022/24 kutokana na jitihada za rais kuinua pato la Taifa na kupunguza hali ya utegemezi.
“Tanzania ni nchi tajiri sana, Tanzania kwa gesi asilia duniani ni nchi ya 82, kwa makaa ya mawe ni nchi ya 50 kwa dhahabu ni nchi ya 22, kwa almasi ni nchi ya 10 kwa helium gesi ni nchi ya kwanza kwa madini ya Tanzanite ni nchi ya kwanza kwa utalii ni nchi ya pili inaifuata Brazil.
“Kwa utajiri kama huu nchi tajiri kama hii kuwa maskini sio sawa sawa hauwezi kuwa unakalia utajiri huu na wananchi wako ni maskini Changamoto tuliyonayo Afrika ni uwezo wa kutumia rasilimali ambazo mungu ametupa kuzibadilisha kuwa fedha zilete maendeleo,” amesisistiza Shigongo.
ZINAZOFANANA
ACT Wazalendo wajifungia kujadili Uchaguzi Mkuu 2025
Dk. Nchimbi awatangazia kiama wanaosaka uongozi kwa kuchafuana na matamko
Gambo awashukia wanaopinga uteuzi wa Samia